Nyoni alicheza mechi hiyo huku akiwa na kadi mbili za njano na sio tatu kama baadhi wanavyodai, kadi hizo alioneshwa kwenye mechi mbili mfululizo zilizopita.
Alioneshwa kadi ya kwanza kwenye mchezo kati ya Mwadui FC dhidi ya Simba (Februari 15, 2018) uwanja wa Kambarage, Shinyanga ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare Mwadui 2-2 Simba.
Kadi ya pili alioneshwa kwenye mechi kati ya Simba dhidi ya Mbao iliyochezwa uwanja wa taifa Dar (Februari 26, 2018) mchezo huo Simba ilishinda 5-0.
Mchezo ambao watu wengi wanadhani Earasto alioneshwa kadi ni kati ya Simba dhidi ya Azam FC (Februari 7, 2018) mechi ambayo ilichezwa uwanja wa taifa, katika mchezo huo ambao Simba ilishinda 1-0 Erasto hakuoneshwa kadi yoyote.
Kwa hiyo mechi ya jana Machi 2, 2018 Erasto alikuwa na sifa zote za kucheza mechi hiyo
0 comments:
Post a Comment