Uongozi wa club ya JKU inayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar wamepokea kwa furaha uteuzi wawacheaji wao wawili kwenye kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kilichotangazwa Machi 8, 2018 kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Algeria na DR Congo.
“Nimefarijika kwa kiasi fulani kwa sababu mpira si lazima wachezaji uwenao wewe mwenyewe wanakaa kwako tu, inatakiwa upate wachezaji wanakwenda kucheza timu ya taifa na kuwakilisha timu zao kupitia timu ya taifa na italeta motisha kwa wachezaji wengine kufanya vizuri”- Saad Ujudi, katibu mkuu JKU.
“Jitihada zao ndio zimefanya waitwe kucheza timu ya taifa kwa hiyo nawaomba wachezaji wetu na wachezaji wa timu nyingine za Zanzibar iwe kigezo kwao ili wao pia wafanye vizuri na kuchaguliwa kwenye timu ya taifa.”
Kikosi cha taifa stars kilichotangazwa machi 8, 2018 kina jumuisha wachezaji watatu wanaocheza ligi kuu ya Zanzibar ambao ni Abdulrahman Mohamed (JKU), Feisal Salum (JKU), Abdulaziz Makame (Taifa Jang’ombe).
Mudathir Yahya (Singida United) na Mohamed Issa (Mtibwa Sugar) ni wachezaji wa Zanzibar wanaocheza ligi kuu Tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment