LIVERPOOL.
UZOEFU. Kwa uwezo waliouonesha Sadio Mane, Roberto Firminho na Mohamed Salah ni wazi kwamba dunia haina mashaka na utatu huu.WANATISHA. Tayari Firminho ameshacheka na nyavu mara 10 sawa na Mo Salah katika CL na pia wameifanya Liverpool kuwa timu yenye mabao mengi katika msimu mmoja wa CL.
Lakini utatu huu haujawahi kucheza fainali yoyote kubwa katika ngazi ya vilabu siku za usoni, tofauti na wenzao wanaokwenda kukutana nao ambao kwao fainali imekuwa kama utamaduni wao wa kila siku. Salah, Mane na Firminho itabidi waiweke Liverpool mabegani mwao na kuwapa CL yao ya 6.
ULINZI UKO SALAMA? Virgil Van Djik ameshaonesha kwanini alinunuliwa kwa pesa nyingi na Liverpool, tangu atue Anfield mwezi January inaonekana tatizo la ulinzi la Liverpool limeanza kutibika, Dejan Lovren maye amekuwa mtamu sana akiwa pembeni mwa Djik.
Andrew Robertson, Trent Alexendre Arnold wanaifanya Liverpool kuwa timu kamili kwa fainali ya CL, golikipa Loris Karius naye tangu apewe nafasi ya kwanza amekuwa muhimu Liverpool, lakini mashaka yanakuja kwa uwezo wao dhidi ya timu kubwa kama Real Madrid.
SUPER SUB. Benchi la Real Madrid unaweza kumuona Isco, unaweza kumuona Asensio na unaweza kumuona Gareth Bale. Hii ni tofauti kwa Liverpool wanaoonekana kuwa na timu ndogo, Liverpool wanaonekana kutegemea tu wachezaji 11 wa kwanza.
Adam Lallana na Emre Can hii ndio inaweza kuwa mechi yao muhimu kabisa kuibeba Liverpool. Hawa wawili wanaweza kuwa “super sub” na ndio wachezaji ambao kwa kiasi kikubwa wanategemewa kubadilisha mchezo kwa Liverpool kama sub.
REAL MADRID.
Beki ya kushoto. Sina mashaka na Marcelo lakini kitu najua kwa mabeki wa Brazil ni rahisi KUPITA NA KUPITWA. Marcelo ni mlinzi ambaye mara nyingi amekuwa akipanda mbele na hakuwa mzuri katika kufanya marking katika eneo lake la kushoto.
Katika mechi hatua ya 16 PSG waliwafunga Real Madrid kupitia eneo hili, Juventus waliishambulia sana Real Madrid kupitia eneo hili, na kaangalie namna Joshua Kimmich alivyoutumia upande huu kufunga moja ya bao bora la CL dhidi ya Real Madrid, yote 9 lakini 10 huu ndio upande Mo Salah anatumia kufanya mauaji.
Uchaguzi wa XI. Zinedine Zidane amekiri kwamba haelewi nani aanze na nani akae benchi, wachezaji wengi wa Real Madrid wanaonekana kuwa fiti sana kuelekea mchezo huu na hili ni tatizo kwa Zizzou hajui yupi amuweke na yupi amuache.
Nafasi 8 za mwanzo za Keylor Navas, Dani Carvajal, Sergio Ramos, Raphael Varane, Marcelo, Kroos, Luka Modric na Ronaldo ziko wazi ni lazima wacheze, kazi inakuja kwa Casemiro, Kovacic, Isco, Gareth Bale, Marco Asensio, Lucas Vazquez na Karim Benzema ambapo lazima watatu wakae benchi.
Kama Zidane atahitaji kukaa na mpira muda wote na kuwa na possesion kubwa baasi Isco na Benzema wataanza katika mchezo huu, Zizou akitaka kukimbizana na Liverpool Bale na Asensio wataanza, na kama atahitaji mtu wa kutembea na Salah ni wazi Lucas Vazquez anaweza kuanza.
Kujiamini. Kwa namna ambavyo Real Madrid wameingia fainali ni wazi kwamba inawapa imani kubwa kushinda mchezo huu, lakini pia kushinda michuano ya CLara mbili mfululizo kunaweza kukawaaminisha kwamba wao ni wababe wa fainali.
Liverpool hawana uzoefu kabisa na fainali hizi lakini hii inaweza kuwa chachu kubwa sana kwao na kuwapa njaa ya kutaka kuionesha dunia kwamba wao pia wanaweza, na kuwa “under dogs” inaweza kuwasaidia kujituma sana mbele ya Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment