Thursday, May 24, 2018


Ukiacha kombe la dunia  wiki hii habari kubwa sana ni mchezo wa Jumamosi kati ya Liverpool na Real Madrid. Zinedine Zidane anataka kuwa kocha wa kwanza katika historia kubeba CL mara 3 mfululizo na Klopp akitaka CL yake ya kwanza kabisa.
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque’s ametoa maoni yake kuelekea katika mchezo huu, maoni ambayo mashabiki wengi wa Liverpool wanaonekana kutoyafurahia.
Vicente del Bosque’s amesema katika kikosi cha Liverpool hakuna mtu anayeweza kupata namba katika kikosi cha Real Madrid, “sio hata Mo Salah anayeweza kupata namba Real Madrid, Gareth Bale na Karim Benzema wako vizuri zaidi” amesema Vicente del Bosque’s.
Kuhusu mchezo wa Jumamosi kati ya Real Madrid vs Liverpool, “Real Madrid wana kikosi kikubwa na bora sana barani Ulaya, naamini siku ya Jumamosi watashinda bao 4-1 na sina mashaka katika hilo.”

0 comments:

Post a Comment