KLABU ya Arsenal jana imetangaza udhamini wa miaka mitatu wa Rwanda kujitangaza kwenye mikono ya jezi za Washika Bunduki hao.
Huo utakuwa mkataba wa kwanza rasmi wa Arsenal kwenye mikono ya jezi, ambako kutaandikwa Tembele Rwanda.
Mkataba
huo ni maalum kuitangaza Rwanda amabyo inaibukia kuwa kituo kikubwa cha
utalii, nchi ambayo uchumi wake unakua kwa kasi barani Afrika.
Tembele
Rwanda itabandikwa kwenye jezi za mikono ya aina yote za Arsenal
kuanzia msimu ujao na juzi zilizinduliwa rasmi katika hafla maalum ya
wadhamini wao wa jezi, Puma.
Mkataba huo wa dau zuri utafanya pia mradi wa Tembele Rwanda kuwa washirika wakuu wa klabu hiyo ya Kaskazini mwa London.
Arsenal imetangaza udhamini wa miaka mitatu na kampeni ya Tembelea Rwanda PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment