Meneja mpya wa
Arsenal Unai Emery amesema anataka klabu hiyo kuwa miongoni mwa klabu
bora zaidi Ulaya kwa mara nyingine, na hata bora duniani.
Alisema hayo alipohutubiwa wanahabari kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa kuwa mrithi wa Arsene Wenger.Mkufunzi huyo wa miaka 46 aliwasilishwa rasmi kwa mashabiki na wanahabari Jumatano kabla yake, akiandamana na afisa mkuu mtendaji Ivan Gazidis kuhutubia waandishi wa habari waliokuwa wamefika kwa wingi.
Alisema: "Ufanisi msimu ujao utakuwa bado tunaukuza, lakini kwa jinsi gani? Kwa kupigania kila taji.
"Hilo limo ndani ya historia ya Arsenal na yangu mwenyewe."
Arsenal walishindwa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2017 na hawatashiriki michuano hiyo msimu wa 2018-2019. Awali, walikuwa wamefuzu kila mwaka tangu 1998.
Mhispania huyo
Gazidis alifichua kwamba Mhispania huyo alikuwa kwenye orodha ya wakufunzi wanane ambao walikuwa wamewekwa kwenye mizani kumtafuta mtu wa kumrithi Wenger, lakini yeye ndiye aliyekuwa naatafutwa zaidi.
"Wote wanane walishiriki mahojiano ya kina na hakuna hata mmoja aliyejiondoa kwenye mchakato huo," Gazidis alisema.
Aliongeza kwamba kazi hiyo ni moja ya zinazotutia zaidi katika ulimwengu wa soka.
"Tuna bahati sana kumpata mtu tuliyemtafuta tangu awali.
"Mahojiano yetu ya kwanza tuliyafanya mnamo 25 Aprili na ya mwisho tuliyafanya 15 Mei. pendekezo la mwisho kwa bodi lilitolewa likiambatana na barua ya kurasa 100 yenye maelezo ya kina.
"wanachama wote wa bodi walifurahia uamuzi wetu."
0 comments:
Post a Comment