Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, kimewasili Alhamis ya leo nchini kikitokea Mali kushiriki mchezo wa kuwania kufuzu fainali za vijana za AFCON (U20).
Ngorongoro wamerejea nchini baada ya kupoteza dhidi ya Mali kwa jumla ya mabao 6-2 uliopigwa jijini Bamako.
Kikosi hicho kiliweza kuruhusu mabao 2-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika hapa nchini kwenye Uwanja wa taifa, Dar es Salaam, kabla ya kwenda Mali na kuambulia kipigo kingine cha 4-1 na kufanya idadi ya mabao kuwa 6-2.
Kipigo hicho kimewaondoa moja kwa moja Ngorongoro Hereos kuwania tiketi ya kucheza mashindano hayo mwakani hivyo safari nyingine ya maandalizi itabidi ianze upya.
0 comments:
Post a Comment