Wednesday, May 23, 2018

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe ametoa onyo la mwisho kwa viongozi wa vyama vya ngumi za kulipwa vya PST na TPBO kurekebisha mwenendo wao, vinginevyo atavifungia.
Mwakyembe ametoa onyo wakati shughuli ya kukabidhiwa taarifa ya Kamati aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza uendeshaji wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini, iliyofanyika jijini Dar es salaam leo May 22 2018.
Mwakyembe amesema kabla ya kuunda kamati hiyo alikuwa na malalamiko mengi kuhusu mchezo wa ngumi za kulipwa kutoka kwa wadau, na alibaini kuna mambo kadhaa ambayo yamekua yakiwadhalilisha mabondia pindi wanapokwenda nje ya nchi, huku wadau wachache wakinufaika na madhabiki hayo.

0 comments:

Post a Comment