Wednesday, May 23, 2018


Kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate leo May 22 2018 ameamua kumtangaza mshambuliaji wa club ya Tottenham Hotspurs ya England Harry Kane kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya England katika michuano ya Kombe la Dunia 2018 inayofanyika Urusi.
Gareth Southgate kabla ya leo kutangaza kuwa Harry Kane kuwa nahodha wa England alikuwa kashatangaza kikosi cha wachezaji 23 wa England wataokwenda World Cup na kuwaacha golikipa Joe Hart na Jack Wilshere, leo ametaja sababu ya kumchagua Harry Kane kuwa nahodha.
“Harry Kane ni mchezaji proffesional sana na hiko ni moja kati ya vitu muhimu ambavyo nahodha anatakiwa kuwa navyo lakini bila shaka Harry Kane atahitaji sapoti kutoka kwa wachezaji wengine ambao nao ni viongozi wazuri ambao wanamzunguuka”>>> Gareth Southgate

0 comments:

Post a Comment