Si hitaji kumpunguzia chochote Mo bilashaka yeye ni mchezaji wa kiwango cha Dunia msimu huu. Lakini Ronaldo amekuwa akionyesha kiwango bora miaka yote na amekuwa akithibitisha hilo msimu hadi msimu.
Ni tumaini langu Salah anaweza kufanya hivyo, na natumainia kufanya hivyo. Bado anaumri mdogo na bado anamuda wa kuwa bora zaidi na zaidi.
Liverpool inatarajia kuikabili Real Madrid kwenye mchezo wa fainali wa michuano ya klabu bingwa Ulaya utakao pigwa siku ya Jumamosi huku Dunia ikiwashuhudia wachezaji Salah na Ronaldo wakikutana uso kwa uso.
Ronaldo amefunga jumla ya mabao 42 katika mashindano yote msimu huu ilihali Salah akitupia 44 msimu kwenye msimu wake wa kwanza Anfield, lakini kipa wa timu hiyo, Karius anaamini kuwa ni mapema mno kwa mshambuliaji wake kumlinganisha na mhezaji huyo bora wa Dunia.
0 comments:
Post a Comment