Wednesday, May 23, 2018

Mkali wa Bongofleva Alikiba na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta wote kwa pamoja wameamua kuwa mabalozi wa elimu wa kujitolea.

Alikiba na Samatta wote wameungana kuhakikisha June 9 2018 watacheza mchezo wa hisani uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa ajili ya kuchangia elimu ambapo pesa zitakazopatikana zitaenda kusaidia maeneleo ya elimu nchini.

Kama unajiuliza itakuwaje siku hiyo? basi Samatta ataunda timu yake ya mastaa wa soka na Alikiba pia ataunda timu yake akichagua mastaa wake, mapato ya mlangoni yataenda kuchangia maendeleo ya elimu nchini.

0 comments:

Post a Comment