RASMI: Yanga yapigwa bao saini ya Salamba
Kwa sasa picha ya Adam Salamba akisaini mkataba na ile akiwa pamoja na Mohamed Dewji Mo ndiyo ina-trend kinoma kwenye social networks kwa upande wa soka.
Unaambiwa tayari Simba wamesha maliza mchezo kwa mshambuliaji huyo aliyekuwa Lipuli ya Iringa. Simba wameipiga Yanga bao la kisigino kwa kuzunguka mlango wa pili na kumaliza biashara.
Yanga ndio walianza kuonesha nia ya kuhitaji saini ya Salamba mapema sana, baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika, kanuni zinawaruhusu kuongeza wachezaji watatu kuimarisha kikosi chao.
Uongozi wa Yanga uliandika barua Lipuli wakimuomba Salama aitumikie Yanga kwenye mechi za kimataifa lakini ombi hilo liligonga mwamba.
Wakati Yanga wakipigwa chini maombi ya kumtumia kwenye mashindano ya CAF, leo mahasimu wao Simba wamefanikiwa kumsajili Adam Salamba kutoka Lipuli FC kwa dau linalotajwa kufikia millioni 40.
Amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba kuanzia msimu ujao.
Simba wanamkumbuka Salamba baada ya kuwafunga kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Samora ambapo bao la kusawazisha la Laudit Mavugo liliinusuru Simba na kichapo.
0 comments:
Post a Comment