Tuesday, May 29, 2018



Ni wiki mbili tu sasa zimebaki ili kuanza mashindano makubwa sana ya soka duniani pale nchini Urusi, mimi binfsi katika tukio ambalo siwezi kulisahau katika michuano ya kombe la dunia ni namna Ghana walivyoikosa nusu fainali 2010.
Katika pita pita zangu leo asubuhi nimekuta pia waziri mwenye dhamana ya mazingiria mheshimiwa January Makamba akikumbushia dhuluma ya makusudi Luis Suarez aliyowafanyia Ghana ili Uruguay wapite.
Kupitia ukurasa wake wa twitter mheshimiwa Makamba alikumbushia tukio la Champions League namna Ramos alivyomuumiza Salah, na akahusianisha na namna Suarez alivyofanya ukatili mwingine dhidi ya Waafrika 2010 kwa kudaka mpira makusudi uliokuwa ukienda kambani.
Lakini wakati Makamba akiwaza hivyo, nahodha wa timu ya taifa ya nchini Uingereza Harry Kane naye kuna jambo hatakuja kusahau kamwe, Kane yeye sisi tukimuwaza Suarez bado ila kwake hamsahau Ronaldinho Gaucho.
“Ilikuwa mwaka 2002 nakumbuka nilikuwa mdogo ila siwezi kusahau namna ule mpira Ronaldinho alivyouweka pembeni kwenye goli, bado inaniumiza lakini ile ni kati ya mambo ambayo yalinifanya nitamani sana kucheza kombe la dunia” alisema Harry Kane.
Herve Renard ambaye kwa sasa ni mwalimu katika timu ya taifa ya Morocco naye pia ana jambo ambalo linamuumiza na kamwe hawezi kulisahau katika maisha yake japo lilimfundisha jambo kubwa.
“Ilikuwa mwaka 1982, wakati Ufaransa tumepoteza dhidi ya Ujerumani na tukafungwa kwa penati, nilijawa na uchungu lakini hali ile ilinisaidia sana kuelewa kwamba kwenye mpira kuna nyakati chungu ambazo unapaswa kuvumilia”
Lipi tukio lako unalokumbuka zaidi katika michuano ya kombe la dunia? Share kumbukumbu yako katika sehemu ya comment.

0 comments:

Post a Comment