Tuesday, May 29, 2018


Waarabu ni watu wenye msimamo mkali. Baada ya Ramos kumuumiza Salah katika mchezo wa klabu bingwa, Waarabu wamesema hapana…. Hili jambo lisiishe hivi hivi. Wamesema hawajali kama mambo ya FIFA hayapelekwi mahakamani au lah wao wanataka mpunga.

Wakili mmoja kutoka Misri ameamua kumtia Ramos mahakamani kwa kile anachodai kuwa Salah hakutendewa haki. Wakili huyu amedai fidia ya takribani €1 billion (£873m/$1.2bn) hii ni takribani trion mbili mpaka 3 za kibongo.
Wakili huyu amesema hili suala sio la kufumbia macho kabisa. Katika udukuzi wangu mitandaoni kuna mambo kadhaa nimeona. Kwanza Salah walio wengi wanamuita Mfalme wa Misri. Lakini Sergio Ramos ameamua kujiita yeye ndo mfalme wa wafalme. Ameendika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba Yeye na Perez hakuna mfalme aliye juu yao.

Mbaya zaidi nmeona Tony Kroos akimtakia Kila la Kheria Mo Salah lakini kwakweli mimi sijaona mahali Ramos ameomba radhi au kumtakia Salah lolote.
Salah alianguka vibaya baada ya mvutano na Ramos. Alipata maumivu makala mkono wale wa kushoto baada ya kuulalia.

Hata Hivyo Mo Salah ameondoa wasiwasi kwamba hilo halitamzuia kucheza kombe la dunia.
Licha ya kwamba Salah ametangaza kuwa ataluwa fiti hili bado halimuungii akilini wakili huyu msomi bwana Bassem Wahba.

alipohojia wa na kituo cha Sada El-Balad , Wahba amesema anakwenda FIFA kwanza kumshitaki Ramos. Kwanza kwa kumuathiri kisaikolojia na kimaumbile mchezaji pendwa na tegemezi wa taifa hilo. Amesema taifa zima lilikuwa macho kumtazama Salah leo anatokea mtu mmoja na kuzima ndoto za wamisri wote. hilo kwake halikubaliki.

“Nimeshafungua Kesi, Ramos alidhamiria kwa makusudi kabisa na nimewaambia FIFA warudie mkanda wa video kwa kina watagundua kuna njama. Nimeomba Fidia bilioni 1”
Wadau wengi wamemlalamikia Sana Ramos. Ramos alionekana kumfanyia kitendo hicho hicho Sadio Mane lakini hakufanikiwa. Pia alionekana kumpiga Karius kiwiko cha usoni lakini mwamumizi hakuliona tukio hilo. Ramos huyu huyu katika pambano hili wakati Salah anatoka nje alionekana kufurahia tukio lile.

Ramos ameshinda UCL lakini ameonekana kupoteza heshima kubwa kwa wadau wa soka pote duniani. Bila shaka huenda akachukuliwa hatua makhususi na FIFA. Namna ya kumsaidia Salah ni manahodha wa timu mbalimbali kuhakikisha kuwa Mo Salah anafika angalau hatua ya 3 bora wa wachezaji bora duniani. Kwa hakika Ramos alitia kitumbua cha Wamisiri mchanga

0 comments:

Post a Comment