Mshambulijai wa
Liverpool Mohamed Salah anasema kuwa hataondoka katika klabu hiyo
mwisho wa msimu huu. Raia huyo wa MIsri mwenye umri wa miaka 25
amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Real Madrid (Mirror)
Kiungo
wa kati wa Ivory Coast Yaya Toure, 34, atakataa maombi kutoka China na
mashariki ya kati kuendelea kucheza kwa kiasi kidogo cha fedha katika
ligi ya Uingereza wakati atakapoondoka Manchester City mwisho wa msimu
huu. (Mail)
- Eric Cantona kurudi Old Trafford
- Gor Mahia kucheza dhidi ya Hull City Kenya
- Barcelona yawika huku Real Madrid ikilazwa

Mkufunzi wa timu ya Uingereza Gareth Southgate anapima kumshirikisha beki wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, 19, na winga wa Fulham Ryan Sessegnon, 17, katika kikosi chake cha wachezaji 35 cha kombe la dunia (Telegraph)
Juventus inajiandaa kuwasilisha ombi la £15m kwa klabu ya Chelsea ili kumnunua mshambuiliaji Alvaro Morata, 25, kwa mkopo. (Express)
Klabu mpya iliopandishwa katika ligi kuu ya Uingereza Wolves imemuorodhesha wa kwanza katika usajili wake mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Andre Silva mwisho wa msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anadaiwa kugharimu £33m. (Sun)
Wolves inajiandaa kuwasilisha ombi la £30m kumsajili kipa wa Sporting Rui Patricio, 30, huku mchezaji huyo wa Ureno pia akisakwa na Napoli.(Diario de Noticias, via Birmingham Mail)
Mshambulaji wa Bournemouth Jermain Defoe amesema kuwa yeye mchezaji mwenza wa Uingereza Wayne Rooney walikuwa wamechoshwa na kombe la dunia la 2010 World hadi wakalazimika kutazama harusi ya Rooney katika DVD. (ESPN)
Kipa wa Manchester City Ederson ameshinda rekodi ya dunia ya Guinness kwa kupiga mpira kwa urefu wa mita 75.35 (FourFourTwo)
Kungo wa kati wa Manchester United anyestaafu Michael Carrick anasema kuwa mkufunzi Alex Ferguson alikuwa akimchezesha wakati wa mvua. (ESPN)

0 comments:
Post a Comment