Mchezaji wa zamani
wa Manchester United na Ufaransa Eric Cantona anatarajiwa kurudi katika
uwanja wa OLd Trafford mnamo mwezi Juni.
Atacheza katika uwanja wa Manchester United katika mechi ya hisani ya shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto Unicef.Raia huyo mwenye umri wa miaka 51anasema kuwa: Hakuna mahali pazuri kama nyumbani .
- Gor Mahia kucheza dhidi ya Hull City Kenya
- Barcelona yawika huku Real Madrid ikilazwa
- Atletico 'imechoshwa' na kero la Barcelona

Itakuwa mara ya kwanza kwa yeye kucheza katika uwanja huo tangu 2001.
''Ninarudi kuhakikisha kuwa mechi hiyo ya Juni 10 ndio bora zaidi na nataka mujiunge nami'', alisema raia huyo wa Ufaransa.
"Njooni tuweke historia katika uwanja wa OLd Trafford kwa mara nyengine ya mwisho''.
Atakabiliana na kikosi cha Uingereza kitakachoongozwa na mwanzilishi wa soka ya hisani Robbie Williams.

Wachezaji wengine wa kikosi hicho cha dunia watakuwa Yaya Toure, Clarence Seedorf, Robert Pires , Jaap Stam na Patrick Kluivert.
Watakabiliana na David Seaman, Jamie Redknapp, Danny Murphy na Robbie Fowler kwa upande wa kikosi cha UIngereza.
Cantona ambaye alijiunga na klabu ya Manchester United kwa dau la £1.2m in 1992 - alifunga mabao 64 katika mechi 143 za ligi akiichezea Manchester United na kushinda mataji manne ya ligi ya Uingereza pamoja na mataji mawili ya kombe la FA katika misimu mitano.

Alipigwa marufuku kwa miezi minane kwa kisa hicho cha 1995. Tangu astaafu katika soka 1997, Cantona amekuwa akiigiza katika filamu ikiwemo ile ya Elizabeth, French Film na Looking for Eric

0 comments:
Post a Comment