Friday, May 11, 2018

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah' usiku wa Alhamisi amebeba tuzo tatu kutokana na mafaniko yake mwaka huu.
Mkali huyo wa mabao alisafiri kwa ndege maalum ya kukodi kwenda kupokwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (FWA).
Mfungaji huyo wa mabao 43 alikabidhiwa tuzo hiyo akitoka kupokea tuzo nyingine mbili usiku huo, ambazo ni Mchezaji Bora chaguo la Wachezaji na Mchezaji Bora wa Mwaka wa Liverpool.
Mohamed Salah akiwa ameshika tuzo ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo

0 comments:

Post a Comment