MSHAMBULIAJI
wa kimataifa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa Alhamisi ametokea
benchi na kuifungia bao la kusawazisha KRC Genk ikipata sare ya 1-1 na
AA Gent katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa
Luminus Arena mjini Genk.
Samatta aliingia uwanjani dakika ya 54 kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis wakati huo tayari Gent wanaongoza kwa 1-0, bao lililofungwa na mshambuliaji kutoka Japan, Yuya Kubo dakika ya 15 akimalizia kazi nzuri ya kiungo kutoka Georgia, Giorgi Chakvetadze.
Samatta alifunga bao lake dakika ya 66, ambalo linakuwa la kwanza tangu Oktoba 25, mwaka jana alipofunga bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Club Brugge katika Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji, Uwanja wa Luminus Arena pia.
Samatta,
mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za
Tanzania leo amefunga bao lake la 23 katika mechi ya 87 tangu Nahodha
huyo wa Taifa Stars ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kikosi chs KRC Genk; Vukovic, Nastic, Colley, Aidoo/Dewaest dk88, Mata, Seck, Malinovskyi, Pozuelo, Trossard, Ndongala/Wouters dk53 na Karelis/Samatta dk53.
AA Gent : Kalinic, Gigot, Rosted, Verstraete, Chakvetadze (32 'Kalu) (69' Janga), Yaremchuk, Dejaegere, Asare, Bronn, Simon and Kubo (78 'Esiti).
Samatta aliingia uwanjani dakika ya 54 kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis wakati huo tayari Gent wanaongoza kwa 1-0, bao lililofungwa na mshambuliaji kutoka Japan, Yuya Kubo dakika ya 15 akimalizia kazi nzuri ya kiungo kutoka Georgia, Giorgi Chakvetadze.
Samatta alifunga bao lake dakika ya 66, ambalo linakuwa la kwanza tangu Oktoba 25, mwaka jana alipofunga bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Club Brugge katika Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji, Uwanja wa Luminus Arena pia.
![]() |
| Mbwana Samatta akikimbia kushangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha KRC Genk |
Kikosi chs KRC Genk; Vukovic, Nastic, Colley, Aidoo/Dewaest dk88, Mata, Seck, Malinovskyi, Pozuelo, Trossard, Ndongala/Wouters dk53 na Karelis/Samatta dk53.
AA Gent : Kalinic, Gigot, Rosted, Verstraete, Chakvetadze (32 'Kalu) (69' Janga), Yaremchuk, Dejaegere, Asare, Bronn, Simon and Kubo (78 'Esiti).

0 comments:
Post a Comment