Monday, June 11, 2018



1. Moja ya wawakilishi wa bara la Afrika timu ya taifa ya Nigeria watakwenda World Cup kwa mara ya 6, Nigeria wameshakwenda 1994, 1998, 2002, 2010, na 2014. Hakuna timu kutoka Afrika ambayo imekwenda michuano hii mara nyingi kama wao.
2. Oscar Tabarez ni kocha wa timu ta taifa ya Uruguay, bwana huyu alikuwepo katika kombe la dunia la mwaka 1990, 2010, 2014 na mwaka huu, kwa taarifa tu ni kwamba hakuna kocha ambaye amewahi kuwepo katika kombe la dunia mara nyingi kama Tabarez kati ya makocha wote wa mwaka huu.
3. Timu ya taifa ya Peru inakwenda katika michuano hii kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1982, hili ndio gepu kubwa la miaka tangu mara ya mwisho kushiriki katika timu zote 32 zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu.
4. Timu ya taifa ya Brazil itakuwa inashiriki kombe la dunia kwa mara ya 21, Brazil ndio timu pekee katika michuano hii ambayo imeshiriki kombe la dunia kwa mara zote tangu mwaka 1930.
5. Timu ya taifa ya Ujerumani ndio timu ambayo inaongoza kwa kuwa na wafungaji hat-trick nyingi katika historia ya kombe la dunia, Edmund Connen, Max Morlock, Heinz Rummeinige, Gerd Muller, Miroslav Klose na Thomas Muller wanafanya timu hii kuwa na wafungaji sita.
6. Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1966 wakati wa michuano ya Euro, hii ndio mara ya kwanza kwa timu ya taifa ya Ufaransa kuenda katika michuano mikubwa bila uwepo wa mchezaji kutoka Arsenal.
7. Timu ya taifa ya Hungary ndio timu yenye rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo wa kombe la dunia, waliipiga El Salvador mabao 10-1 katika mchezo huo ambao ulikuwa katika fainali za kombe la dunia 1982.

0 comments:

Post a Comment