Beki wa kimataifa wa
Gambia anayecheza club ya
KRC Genk ya
Ubelgiji Omar Colley baada ya kuripotiwa kugoma kusaini mkataba mpya ndani ya club ya
Genk na kushinikiza uhamisho wake wa kwenda kucheza soka
Italia katika club ya
Sampdoria iliyomaliza Ligi Kuu nafasi ya 10 msimu wa 2017/2018.

Colley na Samatta wakifurahia goli Europa League
June 10 2018 ameonekana akiwasili nchini
Italia kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya na kukamilisha usajili wake katika club ya
Sampdoria ya Ligi Kuu
Italia Serie A,
Colley ambaye amekuwa akiunda safu nzuri ya ulinzi ya
Genk inadaiwa uhamisho wake wa kujiunga na
Sampdoria utakamilika ndani ya saa 48 kutokea sasa.

Omar Colley na Samatta wakishangilia goli kwa kuabudu kwa imani yao ya dini ya kiislam
Colley atauzwa kwa kiasi kinachoanzia euro milioni 6-8 kutoka
Genk kwenda
Sampdoria,
Genk wanahitaji euro milioni 8 wakati
Sampdoria wakifikia euro milioni 6, kama utakuwa unakumbuka vizuri
Omar Colley na
Mbwana Samatta ambao wamekuwa wakicheza
Genk pamoja kwa miaka miwili sasa, wamekuwa na uhusiano mzuri, kiasi cha kuonekana sehemu mbalimbali wakiwa pamoja.

Omar Colley
Hata hivyo
Omar Colley ambaye ana mkataba na
Genk
wenye kipengele cha kuongeza miaka miwili zaidi, ameonesha dhamira ya
dhati ya kuhitaji kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine, ripoti
zaidi zinaeleza kuwa
Genk na
Sampdoria wamefikia makubaliano na kutaka kuwekwa kipengeleza cha kufaidika kwa asilimia flani kwa mauzo ya
Omar Colley kama akiuzwa kutoka
Sampdoria kwenda timu nyingine.

Mbwana Samatta na Omar Colley wakiwa Macca Saudi Arabia
Omar Colley ni room mate wa
Mbwana Samatta kitu ambacho kimewafanya wawe karibu kwa kiasi kikubwa,
Samatta na
Colley hivi karibuni pia walionekana
Macca Saudi Arabia wakiwa pamoja katika ibada ya umrah, fahamu kuwa sio
Sampdoria pekee walionesha nia ya kumuhitaji
Colley bali hata vilabu vya
Everton,
Hull Cit,
Monaco na
Hamburg ambavyo na vyenyewe vilikuwa vikihitaji huduma ya
Colley.

Msimamo wa Serie A ilivyomaliza Sampdoria
0 comments:
Post a Comment