Ronaldo amefunga bao hilo kunako dakika ya nne kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo huo uliyopigwa kwenye dimba la Luzhniki kumalizika kwa matokeo ya Ureno 1 – 0 Morocco.
Kwa bao hilo linamfanya, Ronaldo kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kimataifa kuliko mchezaji yeyote yule barani Ulaya katika historia ya mchezo wa soka na matokeo ya leo yanaiweka Ureno kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hii baada ya kujikusanyia alama nne kwenye michezo yake miwili.
0 comments:
Post a Comment