Kuelekea fainali ya Kombe la
Shirikisho nchini ASFC, itakayopigwa kesho kati ya Mtibwa Sugar na
Singida United, timu hizo zimejiwekea rekodi ya pekee ambapo kila timu
haijapoteza mchezo kwenye michuano hiyo.
Singida United na Mtibwa Sugar zilianzia hatua ya 64 bora ambapo zilishinda mechi zake na kuingia hatua ya 32 ambapo pia zilishinda kabla ya kucheza robo fainali ambapo Mtibwa iliitoa Azam FC na Singida United ikaitoa Yanga.
Katika nusu fainali Singida United iliitoa JKT Tanzania na Mtibwa Sugar wakaitoa Stand United. Hata hivyo Singida United imeifikia rekodi ya Mbao FC ambayo ilipanda msimu wa kwanza na kufika fainali ya kombe hilo.
Mchezo wa fainali kesho utapigwa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, kuanzia majira ya saa 10:00 Jioni na mshindi ataungana na Simba kuiwakilisha nchi kimataifa.
0 comments:
Post a Comment