Monday, June 18, 2018

Mkongwe wa soka wa Argentina Diego Maradona baada ya kusikia kuwa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetangaza kuwa Mexico, USA na Canada wamepewa uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2026, ameeleza kusikitishwa kwake na maamuzi hayo.
Maradona amefunguka na kueleza kuwa nchini za Mexico na Amerika Kaskazini hazistahili kupewa uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2026,  jan June 13 FIFA  walitangaza kuwa nchi za USA, Mexico na Canada ambazo zinatokea bara la Amerika Kaskazini ndio watakuwa wenyeji wa fainali za Kombe la dunia baada ya miaka nane.

Mexico, USA na Canada watakuwa waenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kufanikiwa kupata kura 134 kati ya kura 210 na kuwashinda Morocco  ambao wameambulia kura 65 pekee, Maradona hajafurahishwa na maamuzi hayo.

0 comments:

Post a Comment