Monday, June 11, 2018


Na: DANIEL S.FUTE
RAIS wa Azerbaijan Mheshimiwa Ilham Aliyev, amethibitisha kauli yake kwamba yeye atakuwa mmoja wa viongozi ambaye atahudhuria sherehe za ufunguzi wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.
Fainali hizi ambazo zimepangwa kufanyika nchini Urusi, na zinatarajia kuanza mapema ndani ya wiki hii. Mchezo wa ufunguzi unatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Luzhniki ambao upo katika mji wa Moscow na utapigwa Juni 14.
Lakini mchezo huo wa ufunguzi hauta hudhuriwa na Rais wa Azerbaijan pekee, bali watakuwepo viongozi wengine wa kubwa kutoka mataifa tofauti tofauti.
Viongozi hao ni pamoja na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan, pamoja na wengi ambao wanazidi kuongezeka siku baada ya siku kabla ya fainali hizi kufunguliwa.
Fainali hizi za Kombe la Dunia, zitaanza Juni 14 hadi Julai 15,2018 na zitafanyika katika miji 11 huko nchini Urusi, Miji hiyo ni- Moscow, St. Petersburg, Kazan, Nizhny Novgorod, Saransk, Kaliningrad, Volgograd, Yekaterinburg, Samara , Sochi na Rostov-on-Don.

0 comments:

Post a Comment