Tuesday, June 26, 2018

Leo Jumanne kutakuwa na mechi nyingine ya kundi C kati ya Australia na Peru itakayochezwa katika uwanja wa Flsht Olympic uliopo mji wa Sochi.
Australia: walikuwa na mwanzo mzuri wa mashindano na ilipelekea kukosa pointi dhidi ya Ufaransa baada ya kujifunga goli katika dakika za mwisho na kuambulia pointi moja dhidi ya Denmark, katika mechi iliyoisha 1-1. Kwa hali yoyote wanajua kwamba ushindi tu wa magoli mengi ndo utafanya wawe na nafasi ya kuwashinda Denmark kwenye msimamo wa kundi C na kuingia hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza katika miaka 12. Hivyo Australia wanaomba Ufaransa wamfunge Denmark.
Tim Cahil alikuwa sehemu ya kikosi kilichofanikiwa Ujeruman mwaka 2016, na anaweza kucheza kwa mara ya kwanza katika kombe lake la dunia ambalo litakuwa la mwisho kwake.Anategemea kuanza kutokana na Andrew Nabbouts kuteguka bega ambapo alilipata dhidi ya Denmark. Jamie Maclaren au kijana anayevutia Tomi Juric anaweza kuchukua nafasi ya Nabbout katika safu ya mbele.
Peru: Waamerika ya kusini wameshatolewa tayari baada ya kupoteza mechi yao dhidi ya Ufaransa na Denmark. Kwa hali yoyote watakuws na matumaini ya kumaliza safari yao ya Urussi huku wakitegemea kupata ushindi ili kuweka sifa kwenye timu.
Upande wao utakuwa bila mshambuliaji wao Jefferson Falfan baada ya nchezaji huyo wa Lokomotiv Moscow kuumia kichwa kwenye mazoez. Alikuwa benchi dhidi ya Ufaransa.Hivyo Paulo Guerrero anatakiwa kuendelea kuwa mtu pekee wa Peru katika safu ya ushambuliaji.
Mitazamo ya makocha wa timu zote mbili
Australia: Kocha wa Australia Bert Van Marwijk akizungumza kuelekea kwenye maandalizi ya mchezo;
Najua kwamba Peru ni timu nzuri na wameonyesha hapa Russia. ” Wanacheza kwa hisia, wana hatari zaidi na tunatakiwa kuwa kitu kimoja.
” Mechi ni muhimu kwetu. Tunaichukukulia umuhimu hasa hasa kwa waliotufata hapa na wanaorudi nyumbani, ambao wamekuwa pamoja nasi kwa moyo wote.
Kocha wa Peru Ricardo Gareca amesema
” Mechi ni muhimu kwetu.”
” Tunaichukulia kama ni ya muhimu kwetu.Tunataka kumaliza ushiriki wetu hapa kwa namna yake hasa kwaajili ya mashabiki wetu.
Kumbukumbu
Hii ni mara ya kwanza timu hizi mbili zinakutana, lakini Peru waliwafunga majirani wa Australia, Newzealand katika mechi za kufuzu za kombe la dunia.
Nahodha wa Peru Paolo Guerrero alikuwa anakosa kombe la dunia baada ya kupewa adhabu ya matumizi mabaya ya dawa baada ya kunywa chai iliyochanganywa na Coca leaf lakini adhabu ilipunguzwa kutoka miezi 18 mpaka miezi 6.
Vikosi vinavyoweza kuanza
Australia: Ryan, Risdon, Sainsbury, Milligan, Behich, Jedinak, Mooy, Leckie, Rogic, Kruse, Juric
Peru: Gallese, Trauco, Rodriguez, Ramos, Advincula, Yotun, Tapia, Froles, Cueva, Carillo, Guerrero.

0 comments:

Post a Comment