MABINGWA
watetezi, Simba SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Ligi
Kuu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, maarufu kama Kombe la
Uhai inayoshirikisha vikosi vya pili vya klabu za Ligi Kuu ya Tanzania
Bara baada ya ushindi wa penalty 5-4 kufuatia sare ya 0-0 dhidi ya
Tanzania Prisons viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Robo Fainali nyingine ya leo, Stand United imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ndanda FC, bao pekee la John Lwitiko dakika ya 75 na zote zinaungana na Azam FC na Mtibwa Sugar zilizotangulia Nusu Fainali kwa ushindi wa 1-0 jana kila timu.
Azam FC iliifunga Mbao FC, bao pekee la Paul Peter dakika ya 60 na Mtibwa Sugar iliifunga Ruvu Shooting bao pekee la Abuu Juma dakika ya 55.
Nusu zitachezwa keshokutwa Azam FC ikimenyana na Stand United na Simba SC wakimenyana na Mtibwa Sugar, wakati fainali itakuwa Juni 21.

0 comments:
Post a Comment