Tuesday, June 5, 2018


Simba na Yanga zimepangwa kundi moja kwenye michuano ya CECAFA Kagame Cup 2018 michuano inayotarajia kuanza Juni 28-Julai 13, 2018.
Kundi A: Azam (Tanzania), JKU (Zanzibar), Uganda Reps (Uganda) Kator FC (S. Sudan).
Kundi B: Rayon Sports (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Lydian Ludic (Burundi), Ports (Djibouti)
Kundi C: Yanga (Tanzania), Simba (Tanzania), St. George (Ethiopia),  Dakadaha (Somalia).
Nicholas Musonye amesema ratiba ya mashindano ya mwaka huu yataanza Juni 28 hadi Julai 13, 2018 lakini ratiba ya mashindano imezingatia ratiba ya kombe la dunia. “Tumezingatia ratiba ya kombe la dunia hivyo mechi hizi hazitaingiliana na ratiba za kombe la dunia.”
Mashindano ya CECAFA Kagame Cup yatachezwa katika viwanja viwili, uwanja wa taifa na uwanja wa Azam Complex.
Bingwa wa mashindano hayo atapata dola 30,000 za kimarekani, mshindi wa pili dola 20,000 na mshindi wa tatu dola 10,000.
Mashindano ya Kagame yanadhaminiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame (mdhamini mkuu) lakini Azam TV ndio warushaji rasmi wa mechi zote za mashindano haya

0 comments:

Post a Comment