KIUNGO wa zamani wa Manchester City, Yaya Toure amemlalamikia Pep Guardiola kutopenda kuchukua wachezaji wa Kiafrika.
Toure
aliondoka Man City mwishoni mwa msimu baada ya miaka minane mizuri,
lakini katika msimu wake wa mwisho hakuwa na mahusiano mazuri na
Guardiola na akaanzishwa katika mechi moja tu ya Ligi Kuu England — na
ya mwisho dhidi ya Brighton ambayo haikuwa na maana yoyote.
Na
sasa katika mahojiano na jarida la Ufaransa, mchezaji huyo mwenye umri
wa miaka 35 mawazo yake yamempeleka mbali juu ya Guardiola na kumvisha
hila za kibaguzi.
Yaya Toure amemlalamikia Pep Guardiola kutopenda kuchukua wachezaji wa Kiafrika PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Akizungumza
na jarida la Ufaransa, Toure alisema: "Pep anataka kuwa na wachezaji
watiifu ambao wanailamba mikono yake. Sipendi uhusiano huu. Namuheshimu
kocha wangu, lakini si kitu chake. Wachezaji wengine hawawezi kukubali
hili hadharani, lakini baadhi tayari wameniambia waliishia kumchukia.
Kwa sababu anafanya kazi na kucheza na kichwa chako,".’
Toure
amesema kwamba hakujua kabisa kwa nini hakupewa nafasi msimu uliopita
kiasi cha kuwauliza makocha kwa nini hapangwi wakati alikuwa vizuri
kuliko hao wachezaji chipukizi waliokuwa wanapewa nafasi.
"Nilihisi (Guardiola) alikuwa ana chuki, ananichukuliwa mimi kama mpinzani," alisema Toure.
Toure
ametoa mchango mkubwa kwa Man City kushinda taji la Ligi Kuu ya England
mwaka 2012 na 2014, na aliisaidia pia timu hiyo kutwaa mataji ya Kombe
la FA mwaka 2011 pamoja na kucheza fainali mbili za Kombe la Ligi.
Toure
alisema: "Nataka kuwa mtu aliyetoa hadithi Guardiola. Barcelona,
hakufanya hivi. Alikuwa anaHe just had the akili za kufuata nyayo za
Cruyf. Pep anataka kuchukuliwa mjuvi. Ninapomuona anakuna kichwa chake
kuonyesha anafikiria, inanichekesha mno. ni komedi,".’
Alipokuwa
akitangaza kuondoka kwa Toure mwez Mei, Guardiola alisema: "Hii klabu
imekuwa hivi ilivyo kwa sababu ya wachezaji kama Yaya. Tunashukuru kwa
alivyokuwa.’
Toure
alikuwa Nahodha wa timu katika mchezo wa mwisho dhidi ya Brighton.
Alikabidhiwa tiketi ya maisha na jezi iliyowekwa kwenye ngao ikiwa na
namba 316, idadi ya jumla ya mechi alizocheza katika klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment