West Ham wametoa
ofa ya pauni milioni 17.5 kwa mshaabulizi wa Borussia Dortmund raia wa
Ukraine Andriy Yarmolenko, 28 ambaye alijiunga na klabu hiyo ya
Ujerumani mwaka uliopita kwa kima cha pauni milioni 23. (Sky Sports)
West
Ham pia wanatarajiwa kumaliza mpango wa kumwinda aliyekuwa kiungo wa
kati wa Arsenal na England Jack Wilshere, 26, ambaye sasa hana mkataba
siku ya Jumatatu. (Mirror)
Manchester United wana uhakika wa kumsaini mshambulizi wa Chelsea William , 29, wakati ambapo sasa Brazil wako nje ya Kombe la Dunia. (Sun)

Liverpool wamefanya mazungumzo na Aston Villa kuhunusu kiungo wa kati Jack Grealish lakini Tottenham wanasalia klabu bora ya kumasaini mchezji huyo mwenye miaka 22. (Mirror)
Mchezaji wa kimatafa wa Marekani Erik Palmer-Brown, 21, ametolewa kwa mkopo na Manchester City kwa klabu ya NAC Breda kwa msimu mpya. (ESPN)

Mlinzi Kieran Tierney, 21, anatarajiwa kusalia Celtic wakati Everton inaamua ikiwa italipa pauni milion 25 zinazotakuwa na Celtic. (Scottish Sun)
Manchester United wako tayari kutangaza ofa ya milioni pauni 40 kwa mchezaji wa miaka 22 wa PSV Eindhoven, mshambuliaji raia wa Mexico Hirving Lozano siku zinazokuja. (Tuttomercatoweb)
Manchester United bado wanaendelea kumfuatilia mchezaji wa miaka 17 wa Molde Erling Haaland, mtoto wa kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City raia wa Norway Alf-Inge Haaland. (Mail)

Ndugu mdogo wa Eden Hazard' Kylian yuko njiani kuhama Stamford Bridge baada ya mchezaji huyo wa miaka 22 kiungo wa kati raia wa Ubelgiji kujiunga na VVV Venlo ya uholanzi kwa majaribio. (Goal)
Lyon wamewaambia Chelsea kuwa kiungo wa kati Tanguy Ndombele, 21, hatauzwa msimu huu wakati Chelsea wanamtafuta atayechukua nafasi ya N'Golo Kante, ambaye analengwa sana na Paris St-Germain msimu huu. (Express)
0 comments:
Post a Comment