Beki wa zamani wa klabu ya Yanga, Hassan Kessy jana alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi ya Ligi Kuu Zambia.
Tuzo hiyo ameshinda baada ya Nkana Red Devils kukipiga dhidi ya dhidi ya Kabwe Warriors.
Kessy ameshinda tuzo hiyo kwa kuchaguliwa na mashabiki wa timu yake baada ya kuisaidia Nkana Red Devils kushinda mabao 2-0 na kuzawadiwa kwacha 1,000 ambayo ni zaidi ya shilingi 200,000 za Kitanzania.
Kessy alisajiliwa na timu hiyo akitokea Yanga kama mchezaji huru baada ya kushindwa kufikia mwafaka na mabosi wake hao wa zamani kuongeza mkataba mpya.
0 comments:
Post a Comment