Sunday, August 19, 2018


Mwanachama na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji, ameshindwa kuungana na wachezaji wa klabu hiyo kwa ajili ya kujumuika nao kula mlo wa usiku baada ya kufikia kwenye hoteli ya Protea iliyopo maeneo ya Posta, jijini Dar es Salaam.

Yanga iliwasili hotelini hapo ikitokea Morogoro ambako ilikwenda kuweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger kutoka Algeria.

Awali uongozi ulieleza angeweza kufika hotelini hapo kwa ajili ya kujumuika nao lakini imekuwa sivyo na haijajulikana sababu za kushindwa kuwasili kwa Manji ni zipi.

Mbali na kushindwa kuwasili hotelini hapo, Manji anategemewa kuhudhuria mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga itacheza dhidi ya USM Alger majira ya saa 1 jioni leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga itashuka dimbani kukipiga na Alger ukiwa ni mchezo wa mkondo wa pili baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 huko Algiers, Algeria May 7 2018.

Yanga ambayo mpaka sasa ina alama moja pekee mkiani katika Kundi D huku Gor Mahia wakiwa kileleni na alama 8 wakiwaacha USM Alger walio wa pili kwa tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga wakati Rayon Sports ikishika nafasi ya 3 ikiwa na alama 2

0 comments:

Post a Comment