Wednesday, August 15, 2018



Kocha mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amefunguka kuwa kwenye mchezo wao ujao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger ya Algeria wana uhakika mkubwa wa kutamba mbele ya wapinzani wao kutokana na kikosi chake kwa sasa kuwa bora.

Zahera raia wa Congo wik­iendi hii kwa mara ya kwanza atakaa kwenye benchi kuion­goza timu hiyo kwenye michezo yake ya kimataifa baada ya kupata kibali kinachomruhusu kuifundisha timu hiyo.

Hadi sasa Yanga wanabu­ruza mkia wakiwa wa mwisho kwenye kundi lao wakiwa na alama moja pekee baada ya kushuka uwanjani katika mich­ezo minne wakifungwa mitatu na kutoka sare mchezo mmoja pekee.

Kocha huyo ambaye pia ana uraia wa Ufaransa, amesema kuwa kwa sasa wanajiamini wana uwezo wa kushinda mbele ya wapinzani wao kutokana na upana wa wachezaji ambao wamepata vibali vya kucheza michezo ya kimataifa ikiwemo Deus Kaseke na Herietier Makambo.

“Kwa sasa tuna uhakika mkubwa wa kufanya vizuri kwenye mchezo wetu huu wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger, kwani kikosi kime­ongezeka na wachezaji ambao wanaweza kuanza mchezo huu wapo vizuri ukilinganisha na mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Gor Mahia.

“Tuna matumaini makubwa kwamba tunaweza kutumia vizuri wachezaji na wakafanya vi­zuri kwenye mechi hii kwani tuko nyumbani lakini pia tulipitia ma­kosa ambayo tuliyafanya kwenye mchezo wa kwanza tulipocheza nao hivyo hatutarajii kufanya tena kama ilivyokuwa kwa mara ya kwanza,” alisema Zahera.

0 comments:

Post a Comment