Sunday, August 19, 2018


Karibia Ligi Kubwa zote barani Ulaya tayari zimeshaanza msimu mpya wa mwaka 2018/19 na jana usiku tulishudia Ligi Kuu Soka Hispania (La Liga) na Ligi Kuu Soka Italia (Serie A) zikianza kutimua vumbi.
Lionel Messi
Mchezo wa kusisimua wa La Liga ulikuwa ni kati ya Barcelona dhidi ya Deportivo Alaves. Mchezo ambao ulimalizika kwa Barcelona kushinda goli 3-0 .
Lionel Messi akitupia goli 2 peke yake huku la tatu likifungwa na Philippe Coutinho, matokeo ambayo yameifanya Barcelona ikae kileleni kwenye msimu wa La Liga.
Kule Italia nako mchezo mkali ulikuwa ni wa Chievo Verona dhidi ya Juventus, mchezo ambao uliisha kwa Juventus kuibuka na ushindi wa goli 3-2 .
Cristiano Ronaldo
Mchezo huu macho mengi ya mashabiki wa soka ulimwenguni yalikuwa kwa Cristiano Ronaldo ambaye hata hivyo licha ya kupata nafasi nyingi lakini hakuweza kupata goli.
Kule Ufaransa nako wakati Messi akifanya yake Hispania, Kylian Mbappe naye aliwanyanyua mashabiki wa PSG baada ya kutupia magoli mawili dhidi ya Guingamp katika mchezo wake wa kwanza tangu atoke kwenye fainali za Kombe la Dunia .
Mbappe na Neymar Jr
Kwenye mchezo huo PSG waliibuka na ushindi wa goli 3-1 goli lingine la PSG lilifungwa na Neymar Jr kwa njia ya mkwaju wa penati na ndio lilikuwa goli la kusawazisha.

0 comments:

Post a Comment