Meneja
wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho pamoja na kikosi chake
wamejikuta wakipata msaada wa jeshi la polisi baada ya kutua nchini
Uingereza wakitokea kwenye ‘tour’ yao ya maandalizi ya msimu Marekani.
Mourinh
anakuwa meneja pekee aliyebaki msimu huu Uingereza mabaye anapigiwa
upatu kuondoka United kufuatia maendeleo yake kutoridhisha mashabiki
wengi wa timu hiyo.
Vyombo
vya habari vimeripoti kuwa mara baada ya meneja huyo kutua kwenye
uwanja wa ndege wa Manchester wakitokea Marekani walipatiwa msaada wa
polisi wa kuwasindikiza kwa kuhofia vurugu ambazo huenda zingefanywa na
mashabiki wa timu hiyo.
Kwasasa
United imerejea Uingereza kujiandaa na ligi kuu ya Uingereza huku
ikionekana kutokuwa vizuri kwenye kikosi chake msimu huu.
0 comments:
Post a Comment