Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara
klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesafiri kuelekea India kwa
ajili ya matibabu.
Taarifa
zinaeleza kuwa, Mkwasa amesafirishwa kuelekea nchini huko kutokana na
matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Afisa
habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten kupitia mtandao wake wa kijamii wa
Instagram ameandika amemtakia kheri Mkwasa katika safari yake ya India
kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.
Mkwasa alitangaza
kuachia ngazi ya Ukatibu Mkuu hivi karibuni akieleza kuwa hawezi
kuwajibika kuendelea kuitumikia Yanga ili kulinda afya yake.
Mkwasa
ametangazwa kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo mnamo Februari 1 mwaka 2017
na kujaza nafasi iliyoachwa wazi kwa muda mrefu iliyokuwa ikikaimiwa
na Baraka Deusdedith baada ya kuondoka kwa Dkt. Jonas Tiboroha.
Charles Boniface Mkwasa aliyepata nafasi ya kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa aliwahi pia kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kabla ya kuwa kocha wa Taifa Stars.
Charles Boniface Mkwasa aliyepata nafasi ya kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa aliwahi pia kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kabla ya kuwa kocha wa Taifa Stars.
0 comments:
Post a Comment