WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ameseti bao la kwanza na kufunga la pili, timu yake Difaa Hassan El- Jadidi ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya MC Alger katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika usiku huu Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan.
Msuva alianza kwa kumsetia Bilal El Megri kufunga bao la kwanza dakika ya 29, kabla yay eye mwenyewe kufunga la pili dakika ya 75 akimalizia pasi ya Saad Lagrou.
Huo ni ushindi wa kwanza kwa Difaa Hassan El- Jadidi, ambayo sasa inafikisha pointi tano ikiwa imebakiza mechi moja dhidi ya vinara wa kundi TP Mazembe, Agosti 28, mwaka huu.
Msuva ameuanza msimu wake wa pili Difaa Hassan El- Jadidi tangu ajiunge nayo kutoka Yanga SC ya Dar es Salaam Julai mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment