Friday, August 3, 2018


Aliyekuwa beki wa Yanga SC, Hassan Kessy hii leo ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa klabu ya Nkana Red Devils inayoshiriki ligi kuu ya Zambia.

Mapema juzi Kessy alisaini kandarasi ya miaka miwili kama mchezaji huru baada ya kushindwa kufikia makubaliano na mabingwa wakihistoria klabu ya Yanga.

Kessy aliondoka Yanga baada ya wakongwe hao wa ligi kushindwa kumpatia shilingi milioni 50 ambayo aliihitaji kijana huyo kwaajili ya kuingia kandarasi nyingine.

0 comments:

Post a Comment