Gerard Pique ameamua kuachana na soka la kimataifa na kujikita zaidi na klabu yake. Amesema hana mpango wa kurudi tena Spain. Pique alifanya maamuzi mwaka 2016 kwamba mwaka 2018 lazima apumzike.
Amesema amechoka kupigania taifa lake huku baadhi ya mashabiki wakimzomea. Pique ni mmoja wa wachezani waliokuwa wakipigania uhuru wa jimbo la Catalan. Mapema hivi karibuni alikutana na kocha spain bwana Luis Enrique lakini akamweleza hana mpango wa kubadilisha maamuzi yake.
Baada ya mchezo wao kufuzu kombe la dunia dhdi ya Albania in Octoba 2016, amechoka kukejeliwa na kukosolewa kila mara.
Pique, 31, hakusema chochote mara baada ya kombe la dunia kutolewa mapema kabisa katika hatua ya 16 bora.
‘nimeongea na kocha Luis Enrique siku kadhaa zilizopita. Aliniambia atanijumuisha kikosini lakini nikamwambia msimamo wangu upo oale pale.
‘naomba niondoke kwa amani. Nimepigania taifa hili. Nakumbuka vyema mafanikio yetu ya kombe la dunia 2010. Kwa sasa imetosha” Alisema Pique
|
---|
0 comments:
Post a Comment