Hivi majuzi nilibahatika kuona mpambano wa Barcelona dhidi ya Ac Milan na ule wa Barcelona dhidi ya Bocca Juniors.
Kama uliangalia kwa makini uligundua kwamba pale uwanjani palikuwepo na mtoto mdogo alikuwa dimba la kati akivalisha watu kanzu. Nilishangaa sana kumuona mtoto ambaye huku kwetu angekuwa darasa la 7 au kidato cha kwanza.
Nilipomfuatilia mtoto yule nikagundua alizaliwa kule Matadepera, jijini Barcelona, jimbo la Catalonia. Taarifa zinaonesha kuwa alijiunga n klabu ya watoto ya Barcelona mnamo mwaka 2013, akitokea UFB Jàbac Terrassa klabu ya zamani ya baba yake.
Mnamo 24 February 2018, alicheza meci ya wakubwa akimpokea Marcus McGuane in a 1–1 wakati Barcelona ikicheza na Gimnàstic de Tarragonafor kutoka ligi daraja la Segunda
Baba yake mzee, Carlos, was alicheza kama beki wa kushoto katika klabu ya Terrassa FC.
Katika maisha yake pale klabu aliisaidia Barcelona kutwa ubingwa wa UEFA Youth League: 2017–18 akiwa amefunga mabao matatu na kutengeneza mengine matatu.
Mechi yake ya kirafiki dhidi ya Ac Milan alifanya makubwa sana licha ya kupewa dakika 45 tu. Kwa dakika hizo kuna watu walisema kuwa kwa namna anavyogusa mpira ni kama Andrés Iniesta na ana upeo mkubwa wa kufikiri kama legendi mkubwa wa Barcelona Xavi.
Kocha mkuu wa Ernesto Valverde alimwagia sifa nyingi sana bwana mdogo yule kwa uwezo wake mkubwa alipoonesha.
Kwenye mchezo wa Supercopa dhidi ya
Sevilla alikuwepo benchi lakini hakuweza kuanza.
M | G | A | DG | Jumla | ||
---|---|---|---|---|---|---|
13 | 3 | 3 | 320 | 961 | ||
UEFA Youth League | ||||||
10 | 3 | 3 | 300 | 900 | ||
LaLiga2 | ||||||
3 | – | – | – | 61 |
0 comments:
Post a Comment