Friday, August 17, 2018



Manchester United inakataa kumuuza mchezaji wake wa kiungo cha kati raia wa Ufaransa Paul Pogba, anayetaka kuhamia Barcelona. (Sun)

Arsenal ina imani itaendelea kumzuia mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Wales Aaron Ramsey, mwenye umri wa miaka 27, licha ya Barcelona, Lazio na ligi kuu ya Uchina kumwinda. (Mirror)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema anatarajiwa wachezaji wataondoka katika klabu hiyo kabla ya kufika muda wa mwisho wa uhamisho wa wachezaji Ulaya licha ya kuwa timu hiyo haikusajili mchezaji yoyote msiu huu wa joto.(Sky Sports)

Lakini mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham raia wa Ufaransa Moussa Sissoko, mwenye miaka 29, amewaambia mashabiki wake kuwa atasalia katika kalbu hiyo.(Talksport)

Pochettino pia anasema anapanga kuwa na Tottenhamkwa muda mrefu baada ya nafasi ambayo angeweza kujiunga na Real Madrid au Chelsea msimu uliopita. (Mirror)

Chelsea imefanya mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha mbele wa Lyon Nabil Fekir, 25, msimu wa joto lakini ikaamua kutomsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.(Goal)

Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini ametupilia mbalia hatau ya kuhama kwa mchezaji wa Ivory Coast Yaya Toure, ambaye ni ajenti wa bure baada ya kuondoka Manchester City. (Sun)

Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, mwenye miaka 25, anasema ananuia kustaafu soka ya kimataifa baada ya Euro 2020. (Business Insider

Kutoka BBC

0 comments:

Post a Comment