Monday, August 13, 2018


MWANASOKA mstaafu wa Brazil, Ronaldo Lima amewashukuru waliomtakia heri baada ya kuwekwa chumba cha wagonjwa walio kwenye uangalizi maalum katika hospitali moja kisiwa cha Ibiza kutokana na ugonjwa wa  Pneumonia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 imeelezwa aliugua ghafla na kukimbizwa hospitali ya Can Misses visiwani humo Ijumaa jioni.
Pamoja na hayo, Ronaldo ameandika kwenye Twitter Jumapili kuwatuliza watu hofu juu aya afya yake - akisema kwamba ataruhusiwa Jumatatu. "Marafiki nilikuwa nina  homa kali ya mafua ilinipata Ibiza na ikabidi nilazwe Ijumaa, lakini naendelea vizuri. Nitaruhusiwa kesho na kurudia nyumbani. Asanteni wote kwa upendo wenu na ujumbe wenu!,"ameandika. 

Ronaldo Lima amewashukuru waliomtakia heri na kusema kwamba ataruhusiwa kesho 

Taarifa ya Kisiwa chenye kuheshimika mno, Diario de Ibiza imesema kwamba Ronaldo aliomba kuhamishiwa hospitali binafsi, iitwayo kliniki ya Nuestra Senora del Rosario kabla ya usiku mkubwa Ijumaa. 
Ronaldo anayechukuliwa kama mmoja wanasoka wakubwa kuwahi kutokea duniani, anamliki nyumba Ibiza na ni kawaida kwake kuzuru huko.
Inaaminika alikwenda mjini Ibiza kwa mapumzizko ya majira ya joto.
Ronaldo alianguka kwa homa ya dengue Januari mwaka 2012 na akaposti picha yake kwenye Twitter: "Habari za asubuhi kwa wote ambao wameuanza mwaka mpya na Dengue.'
Alistaafu soka mwaka 2011 baada ya kuzichezea kwa mafanikio Barcelona, Inter Milan na Real Madrid.
Ronaldo alistaafu soka akiwa amefunga mabao mazuri 414 kati ya hayo, 62 akiifungia timu yake ya taifa katika mechi 98 alizochezea timu yake ya nchi.
Alifunga mabao manane na akafunga katika kila mechi ya Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002 mbali na Robo Fainali kuelekea kutwaa Kombe hini in Japan. 
Alistaafu akiwa amefunga jumla ya mabao 12 kwenye Kombe la Dunia akiifikia rekodi ya gwiji aliyemtangulia, Mbrazil pia, Pele.

0 comments:

Post a Comment