Kikosi cha Simba leo kimeendelea na mazoezi katika viwanja vya Gymkhana tayari kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii pamoja na kuanza kwa ligi kuu Tanzania Bara.
Kikosi cha Simba leo kinatarajia kusafiri kuelekea mkoani Arusha ambapo kikiwa mkoani huko kinatarajia kucheza mchezo mchezo mmoja wa kirafiki.
Baada ya kucheza mechi hiyo mkoani humo, Simba wataunganisha moja kwa moja kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo dhidi ya Mtibwa utakaopigwa Agosti 18 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Kuelekea mechi hiyo, Nahodha wa kikosi cha Simba, John Bocco ana asilimia 99 ya kutocheza mechi hiyo kutokana na kuendelea kusumbuliwa na majeruhi.
0 comments:
Post a Comment