Monday, August 13, 2018

πŸ†
Klabu ya Barcelona imefanikiwa kutwaa taji la Spanish Super Cup baada ya kuifunga timu ya Sevilla jumla ya magoli 2 – 1 mchezo uliyopigwa Tangier, Morocco.

Katika mchezo huo uliyopigwa nje ya Hispania umeshuhudia Lionel Messi akiweka rekodi yake ya kutwaa mataji mengi zaidi ndani ya timu hiyo kuliko mchezaji yeyote mara baada ya kufikisha idadi ya makombe 33.
Sevilla ilitangulia kupata bao mapema kupitia kwa Pablo Sarabia kisha Barça kusawazisha kupitia kwa Gerard Pique kabla ya Ousmane Dembele kuipatia timu hiyo ushindi kwa goli lake la dakika za mwiaho.
Messi akiwa amevalia kitambaa cha unahodha rasmi akipokea kijiti kutoka kwa Iniesta amefikisha idadi ya mataji hayo 33 na kuweka historia ndani ya klabu hiyo

0 comments:

Post a Comment