Saturday, August 11, 2018


KIKOSI cha Simba SC kimewasili salama wilayani Ruangwa mkoani Lindi leo, tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji, Namungo FC kuzindua Uwanja wa Majaliwa.
Ikiwa ni siku mbili tu tangu watoke sare ya 1-1 na Asante Kotoko ya Ghana katika mchezo mwingine wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba SC kesho watamenyana na Namungo FC ya Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Katika mchezo huo, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Kassim Majaliwa ambaye Uwanja wake ndiyo unazinduliwa. 
Basi la wachezaji wa Simba SC baada ya kuwasili Uwanja wa Majaliwa 
Kocha wa Simba SC, Mbelgiji Patrick J Aussem akizungumza na Mwandishi wa Habari baada ya kuwasili 

Kwa Simba SC, mchezo huo utakuwa sehemu ya maandakizi ya mchezo wake wa Ngao ya Jamii Aggosti 19 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza dhidi ya Mtibwa Suga

0 comments:

Post a Comment