Kwa
mara yakwanza ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1 hapo jana imeanza kutumia
mfumo wa VAR kwenye mchezo wa ufunguzi baina ya timu ya Marseille
iliyopata ushindi wa mabao 4 – 0 dhidi ya Toulouse.
Mchezaji
wazamani wa West Ham, Dimitri Payet amenufaika na VAR baada ya kupewa
penati kupitia mfumo huo na kuandika bao lake lakwanza dakika ya 45
kabla hajafunga lapili dakika ya 62 wakati wachezaji wengine waliyotupia
mabao ni Germain dakika ya 89 na Florent Thauvin akihitimisha karamu
hiyo yamagoli dakika ya 90+2.
Payet ambaye alishindwa kucheza
kombe la dunia kutokana na kusumbuliwa na majeraha amepata penati hiyo
baada ya mwamuzi wa mchezo huo Ruddy Buquet kuamuru kona kabla ya VAR
kumzawadia penati mchezaji huyo.
0 comments:
Post a Comment