Wakala
wa mchezaji Paul Pogba ambaye ni Mino Raiola yupo nchini Uingereza kwa
mazungumzo na klabu ya Manchester United juu ya uamisho wa kiungo huyo
wa Ufaransa.


Klabu
ya Barcelona na Juventus zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya mshindi
huyo wa taji la kombe la dunia, Pogba ambaye siku za hivi karibuni
ameonyesha kutokuelewana na meneja wake Jose Mourinho.

Kwa
mujibu wa Mundo Deportivo, Raiola yupo Uingereza kwaajili ya kufanya
mazungumzo na United juu ya uhamisho wa kiungo huyo wakati dirisha la
usajili nchini humo likitarajiwa kufungwa siku ya Alhamisi.
Barcelona
inahitaji kujenga muunganiko wa Pogba, Philippe Coutinho na Lionel
Messi ili kuhakikisha inaimarisha kikosi chake msimu huu.
Wakati
Juventus baada ya kukamilisha dili la Cristiano Ronaldo lenye thamani
ya pauni milioni 100 imesema kuwa ipo katika mbio za kumsajili Mfaransa
huyo.
0 comments:
Post a Comment