Mamia ya wafanyakazi leo wamechoma moto matairi na kuzingira tawi la kampuni kubwa ya kuunda magari ya Nissan mjini Barcelona baada ya kampuni hiyo kutangaza kuwa itakifunga kiwanda hicho mwezi Disemba.
Kufungwa kwa tawi hilo na mengine duniani ni sehemu ya mpango wa mageuzi unaonuwia kupunguza gharama za uzalishaji kutokana na athari za virusi vya corona.
Karibu wafanyakazi 1,000 waliofunikia nyuso mbali ya kuchoma moto maitiri pia waliifunga kabisia njia kuu ya kuingia na kutoka eneo la kiwanda.
Uamuzi huo wa Nissan ni pigo kubwa kwa Uhispania inayoandamwa na ukosefu wa ajira na kuanguka kwa uchumi kutoka na mzozo wa virusi vya corona.
Kampuni hiyo ya kuunda magari ya Japan, imetangaza kupunguza uzalishaji kwa asilimia 20 kufidia gharama za uendeshaji baada ya kurikodi hasara kwa zaidi ya miaka 11.
0 comments:
Post a Comment