IMEELEZWA kuwa, makocha wote wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu England wameambiwa kwamba wanapaswa kumaliza mechi zao zilizobaki ndani ya wiki sita ili kumaliza shughuli za michezo kwa msimu wa 2019/20.
Tangu Machi 13 hakukuwa na mechi ya ushindani iliyochezwa baada ya kuibuka kwa janga la Virusi vya Corona lililovurugavuruga mambo na kusababisha michezo kusimamishwa.
Kwa sasa tayari timu zinazoshiriki Ligi Kuu England zimeruhusiwa kuanza kufanya mazoezi ya pamoja tofauti na awali ambapo walikuwa wanafanya mazoezi kwa mafungumafungu.
Ligi inatarajiwa kurejea rasmi wiki ijayo ambapo itakua na mwendo kama ilivyo Bundesliga ya Ujerumani ambayo imeshaanza na wanacheza bila uwepo wa mashabiki huku ikitarajiwa kukamilika mapema mwanzoni mwa Agosti.
Miongoni mwa makocha waliopewa taarifa hiyo ni pamoja na Jurgen Klopp wa Liverpool, Mikel Arteta wa Arsenal
0 comments:
Post a Comment