JEREMIE Aliadiere, mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Arsenal amesema kuwa mshambuliaji Pierre Emerick Aubameyang inabidi auzwe mazima.
Nyota huyo amesema Aubameyang amechangia kumuweka Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta njia panda juu yake asijue la kufanya.
"Hakuna namna wanayopaswa kufanya Arsenal kwa sasa zaidi ya kumuuza Aubameyang kwa dau lolote lile iwapowatachelea mpaka mkataba wake uishe ataondoka bure itakuwa hasara kwao," amesema.
Aubameyang alisajiliwa ndani ya Arsenal akitokea Klabu ya Borussia Dortmund na amecheza jumla ya mechi 97 na kufunga mabao 61.
0 comments:
Post a Comment