Klabu
ya soka ya Simba imemtangaza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Kassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi wa siku ya ‘Simba Day’
ambapo timu hiyo itashuka uwanja wa taifa kuwakabili Asante Kotoko ya
Ghana Agosti 8, 2018.
Afisa habari wa Simba, Haji Manara amethibitisha hilo mbele ya waandishi wa habari kuwa tayari Waziri mkuu Majaliwa atakuwa mgeni rasmi siku hiyo.
”Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amekubali ombi letu, na ninaomba nitangaze rasmi
kuwa yeye ndio atakuwa mgeni rasmi kwenye tamasha letu la ‘Simba Day’
akiongoza shughuli zote ambazo zitafanyika siku hiyo,”- amesema Manara.
Manara
amewataka mashabiki wa timu hiyo kutojihusisha na masuala ya kugushi
tiketi kwani wao kama klabu wamejidhatiti kuhakikisha watu wa aina hiyo
hawapati mwanya ndio maana suala la usimamizi wa tiketi uwanjani
wamelikabidhi kwa Suma JKT.
Mabingwa hao wapya wa
ligi kuu huadhimisha siku hiyo ya Simba Day kila ifikapo Agosti 8 ya
kila mwaka kwa kufanya shukhuli mbalimbali za kijamii na kuwatambulisha
wachezaji wao wapya.
0 comments:
Post a Comment